manyaki-1.jpg ...      ...

LULU AFIWA NA MPENZI WAKE

LULU AFIWA NA MPENZI WAKE SIKU YA KUZALIWA KWAKE.
KIFO CHAKE CHAFANANISHWA NA CHA KANUMBA.
Habari zinazoendelea kutufikia kwenye meza yetu zinadai kuwa marehemu Seki aliyefariki ghafla hapo jana ambaye pia anadaiwa kuwa mpenzi wa mwanadada Elizabeth Michael – LULU alikuwa ni mume wa mtu na ameacha mjane na watoto.Kwa mujibu wa mtoa habari wetu huyu marehemu Lusekelo maarufu kama seki alikuwa ni mfanyabiashara hapa mjini mwenye biashara kadhaa na alikuwa na uwezo mzuri tu wa kifedha.
Habari za uhakika zinasema kuwa Chanzo cha kifo cha Bw Seck kilisababishwa na kumuokoa mtoto wake aliyekuwa anaangukia meza, kwa bahati mbaya akaangukia yeye meza hiyo na kumuumiza vibaya sehemu ambayo haijaweza kujulikana na kupelekea kifo chake.
Inasemekana kuwa, Jamaa huyo alikuwa chanzo cha Lulu ku-“move on” na kumsahau Kabisa Kanumba.
Jana ikiwa ni siku ya Kumbukumbu ya kuzaliwa Lulu, ambapo ndugu Seck alifariki dunia hali iliyomchanganya LULU mpaka kufikia kufunga akaunti yake ya Instagram iliyokuwa na “followers” (mashabiki ) zaidi ya laki nne na thelasini na mbili (432,000+).
Mungu Ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.

Previous
Next Post »