NEY WA MITEGO AWEKA WAZI VIPIMO VYAKE VYA DNA HIVI HAPA
Baada ya utata mzito kutawala kwenye vyombo vya habari
juu ya uhalali wa mtoto wa Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa
Mitego’ kwa mzazi mwenzake Siwema Edson, hatimaye kipimo cha vinasaba
(DNA) kimetoka na kumaliza ubishi kwamba mtoto huyo aitwaye Curtis ni
damu halisi ya msanii huyo.
Hivi karibuni, Nay na Siwema ambao walikuwa wapenzi kisha kumwagana,
waligombana na kila mmoja kuzungumza lake juu ya mtoto wao huyo ambapo
Siwema alidai si damu ya Nay wakati msanii huyo alisema ni damu yake.
Licha ya kupokea majibu hayo mazuri kwake, Nay aliyachukua majibu
hayo kwa kuangua kilio cha furaha huku akieleza ya moyoni kuhusiana na
sakata hilo.
“Hili ni swala ambalo lilikuwa linaniumiza kichwa kila
kukicha. Unajua kama mwanaume, mtu akwambie mtoto si wako unadhani ni
maumivu kiasi gani utayapata? Inauma sana, mtu umelea kuanzia mimba hadi
mtoto amezaliwa, si kitu kidogo.
“Namshukuru Mungu kwa majibu kwamba ni damu yangu. Mashabiki wangu
watambue tu kwamba, Curtis ni mwanangu asilimia mia hivyo hakuna ubishi
tena.
“Ujue nampenda sana mwanangu na kwa bahati nzuri huyo ndiye
mwanangu wa kiume pekee, hivyo sikutaka kuruhusu wazo lolote kutoka kwa
mtu mwingine maana hata kama majibu yasingesema kama ni wangu nilikuwa
radhi kuishi naye na kumlea bila kujali hilo kwa sababu tu niliamini
siku zote ni mali yangu,” alisema Nay.
Nay aliingia kwenye utata huo takriban mwezi mmoja uliopita baada ya
kupishana kauli na Siwema ambaye alimfumania akiwa na mwanaume mwingine
nyumbani kwake, jijini Mwanza na kuamua kumchukua mtoto kisha kuishi
naye jijini Dar kwa msaada wa mama yake mzazi.
GWAJIMA, KOVA WAFIKA PATAMU: SOMA HAPA KINACHOENDELEA:
Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,
Mchungaji Josephat Gwajima amekamatwa na Jeshi la Polisi na kwa sasa
yupo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Habari zaidi pamoja na picha kuhusu taarifa hizi zitawajia hivi punde.
Chanzo cha habari kinadai niutajiri wake ndio unaleta maswali mengi kwa waumini wake.