manyaki-1.jpg ...      ...

SHAKIRA AMPELEKA MTOTO WAKE WA MIEZI MIWILI KUTAZAMA MPIRA

SHAKIRA AMPELEKA MTOTO WAKE WA MIEZI MIWILI KUSHUHUDIA BARCELONA UWANJANI.

Ni miezi miwili sasa tangu mwanamama na muimbaji mwenye asili ya Colombia Shakira Isabel Mebarak kujifungua mtoto wake wa pili Sasha lakini tayari mwanamuziki huyo ameshaanza kumtoa mtoto out.
Siku ya jumamosi Shakira alionekana akiangalia mpira akiwa na mtoto wake kwenye mechi kati ya timu ya mpenzi wake Gerard Pique dhidi ya Valencia. Shakira alionekana mwenye furaha na mara baada ya mpira kwisha aliingia uwanjani na kwenda kupiga picha ya pamoja akiwa na mtoto, mzazi mwenzake na baadhi ya wachezaji wa Barcelona.
Shakira na Pique wamedumu kwenye mahusiano yao kwa muda wa miaka mitano sasa wanaonekana wenye furaha kila kukicha. Huyo atakua ni mtoto wao wa pili baada Yule wa kwanza mwenye umri wa miaka miwili wanaemuita Milan.

Previous
Next Post »