manyaki-1.jpg ...      ...

Kumbukumbu ya Amina Ngaluma J’mosi Dar

KISOMO cha kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa mwimbaji mahiri nchini, marehemu Amina Ngaluma ‘Japanese’ kinatarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii Kitunda, Machimbo Dar es Salaam.* Akizungumza baba mzazi wa marehemu, Kassim Ngaluma, alisema kisomo hicho kitafanyika nyumbani kwa wazazi wake marehemu na kuwaomba ndugu, jamaa na marafiki mbalimbali wa marehemu wakati wa uhai wake wahudhurie.“Tunaomba wote tulioshiriki kwa namna mbalimbali wakati wa msiba wa marehemu mwanangu, tushirikiane pia katika kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo chake,” alisema Mzee Ngaluma.
 Amina Ngaluma ‘Japanese’ ENZI ZA UHAI WAKE
Previous
Next Post »