manyaki-1.jpg ...      ...

VYAMA VYA SIASA VYAONDOA IMANI NA NEC JUU YA MAJIMBO YANAYOGAWIWA

Vyama vya siasa nchini Tanzania vimeitilia shaka tume ya taifa ya Uchaguzi NEC katika ugawaji wa majimbo,kukamilika kwa uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, upigaji wa kura ya maoni pamoja na uchaguzi mkuu na kudai kuwa haijaweka bayana juu ya kukamilika kwa michakato hiyo.
Akizungumza kando ya mkutano wa Vyama vya siasa na tume hiyo Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, amesema kuwa mpaka sasa uwezekano wa kufanyika kura ya maoni na uchaguzi mkuu ni jambo lisilowezekana.
Prof Lipumba amesema kuwa muda uliowekwa katika ugawaji wa majimbo na ratiba ya uandikishaji wa daftari la kudumu ni mchache na bado tume haina ratiba kamili ya zoezi zima la ugawaji majimbo na tarehe za uandikishaji katika mikoa iliyobaki.
Previous
Next Post »