Tuzo
za Tanzania zijulikanazo kama Kilimanjaro Tanzania Music Award
zinazofanyika Tanzania zimekuwa na lawama nyingi toka zilipoanza, Tuzo
za KTMA ni Tuzo za pili kwa ukubwa Barani Afrika , Mwaka huu Tuzo hizi
zilifanyika Tarehe 13 June 2015 katika ukumbi wa Mlimani City.
Tuzo hizi zimekuwa zikilalamikiwa sana na watu, kipengele ambacho kinaonekana kuwa na utata ni tuzo ya mtumbuizaji bora na mtunzi bora ambazo zote zilienda kwa Ally Kiba.
Kwa maoni yangu nakubaliana na AY kwa sababu nchi za wenzetu hawatumii kigezo cha watu kupiga kura pekee, huwa kunakuwa na jopo la majaji ambao hukaa na kuchagua kilicho bora. Hili ni jambo la kurekebisha katika tuzo hizi kwa sababu kwa namna moja au nyingine zinakatisha tamaa wasanii wanaochipukia katika muziki.
AY
AY ambae ni msanii wa Kimataifa kutoka Tanzania ametoa maoni yake kuhusu Tuzo hizi. AY amesema “Tuzo
naziona zina ubora na upungufu wake,ila kama ukikubali kushindanishwa
unatakiwa ukubali matokeo, cha msingi nachoona kura za majaji iwe 70% na
watu 30% unajua kwenye tuzo watu hawawezi kukubaliana matokeo asilimia
mia, ila nachoona mimi iwe kama tunzo zingine kuwa 70% majaji na 30%
watu kuepusha kuchakachua kura na kuchagua kilicho bora maana kuna
wakati nguvu ya ushabiki inaharibu ukweli wa matokeo”.Tuzo hizi zimekuwa zikilalamikiwa sana na watu, kipengele ambacho kinaonekana kuwa na utata ni tuzo ya mtumbuizaji bora na mtunzi bora ambazo zote zilienda kwa Ally Kiba.