Jumuia tatu za kikanda zinajiandaa
kuungana kuunda soko huru kubwa barani Afrika. Leo jumuiya ya maendeleo
kusini mwa Afrika, jumuia ya Afrika Mashariki na COMESA, zinatarajiwa
kusaini mikataba ambayo itaruhusu uanzishwaji rasmi wa muungano mpya.
Inakisiwa
kuwa mpaka kufikia mwa 2017, zaidi ya Waafrika million mia sita
watafaidika na mpango huu. meetingMkutano wa maafisa wa biashara nchini
Misri unaendelea huku wakiwa katika hali ya mashaka kukamilisha mpango
huo.Inaarifiwa kuwa mpango huo utakuwa tayari kusainiwa hii leo. Baada ya hapo, mapatano hayo yatazinduliwa rasmi kwenye mkutano wa umoja wa Afrika mwishon mwa juma hili.
Baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, jumuia ya kibiashara ya Afrika itaanzisha soko moja kubwa la pamoja litakalohusisha nchi ishirini na sita.
Lengo la jitihada hizo ni kuondoa vikwazo katika bidhaa ambapo itakuza shughuli za kiuchumi zenye thamani ya kiasi cha dola za kimarekani trilion moja.
Kukamilika kwa mpango huu huko Sharma Sheikh chini Misri itakuwa ni hatua ya awali tu, baada ya hapo mkataba huo utahitajika kuhakikiwa na bunge la kila nchi, kabla ya kuanza rasmi kufanya kazi.
Muungano kwa Afika si jambo jipya. Takribani nusu karne tangu Bara la Afrika lilipojipatia uhuru, serikali zimekuwa zikijadili namna ya kukuza biashara ya ndani.
Miundombinu mibaya kama vile reli, barabara na usafiri wa anga ambapo inaleta ugumu kupitisha bidhaa mipakani. Pia nchi nyingi zinajaribu kulinda viwanda vyao vya ndani.