Utoaji zabuni ya maandalizi ya
kombe la dunia mwaka wa 2026 umeahirishwa kufuatia madai ya ufisadi
katika utoaji wa maandalizi ya kombe hilo mwaka 2018 na 2022.
Katibu mkuu wa shirikisho hilo Jerome Valcke amesema kuwa ni 'ujinga' kuanza mpango huo katika mazingira yaliopo.Kura ya kumtafuta atakayeandaa kombe la dunia mwaka 2016 inatarajiwa kufanyika mjini Kuala Lumpur mwezi May mwaka 2017.
Marekani iko kifua mbele kuandaa michuano hiyo lakini Canada,Mexico na Colombia pia zimewasilisha ombi la kutaka kuandaa.
Urusi na Qatar walichaguliwa kuandaa michuano ya mwaka 2018 na 2022 kupitia kura ya siri iliopigwa na wanachama wakuu wa FIFA wapatao 22 mnamo mwezi Disemba mwaka 2010.
Lakini viongozi wa mashtaka nchini Uswizi wanachunguza madai ya ufisadi yanayozunguka zabuni hizo.