manyaki-1.jpg ...      ...

WEMA SEPETU AFUNGUKA SABABU YA KUTOMPIGIA DEBE DIAMOND PLATINUMS KWENYE TUZO ZA KILI

 Akifunguka kupitia 255 ya XXL,Wema alisema kuwa Ali Kiba alimuomba ampigie debe kwenye akaunti yake ya Instagram,kwani hata msanii huyo aliwahi kumpigia debe alipowania tuzo za Watu ndiyo maana alifanya hivyo.
Staa wa filamu za Kibongo,Wema Sepetu ametajwa kuwa ndiye aliyechangia kwa kikubwa  ushindi wa tuzo tano za Killi za msanii wa Bongo Fleva,Ali Kiba kutokana na kumpigia debe mara nyingi kupitia akaunti yake ya Instagram.

 Hata hivyo alipoulizwa mbona hakumpigia debe aliyekuwa mpenzi wake,Diamond Platinum ambaye ni hasimu wa msanii Ali Kiba,alisema kuwa Diamond hakuwahi kumuomba ampigie debe kama angemuomba angefanya hivyo kwani hana tatizo na msanii huyo.
‘’Sina tatizo na Diamond kama angeniomba nimpigie debe Instagram ningefanya hivyo,’alisema Wema.
Wema Sepetu afunguka sababu ya kutompigia ‘debe’ Diamond kwenye tuzo za Kili.


Previous
Next Post »