Baraza la kikatiba la Hong Kong limeanza kujadili mpango wa mageuzi ya kisiasa kabla ya kupigiwa kura baadaye wiki hii.
Mapendekezo
yao ni kuwa wakaazi wa Hong Kong wataweza kumpigia kura kiongozi wao
katika uchaguzi wa mwaka wa 2017 japo wagombea wote kwanza lazima
waidhinishwe na serikali kuu ya China .Watetezi wa demokrasia wameshutmu hilo kuwa demokrasia ya longo longo.
Tayari mamia ya watetezi hao wamekusanyika nje ya afisi za baraza hilo wakibeba mabango na kutoa maneno ya kutukana baraza hlo.
Lakini wanaoungamkono mpango huo kutoka Beijing wanasema kuwa Hong Kong kwa sasa inahitaji uthabiti na wametoa wito kwa wabunge hao wapitishe pendekezo hilo.