15 Julai 2015
Jumba
la Westgate jijini Nairobi nchini Kenya lililoshambuliwa na magaidi wa
Alshabab miaka miwili iliyopita linatarajiwa kufunguliwa upya mwishoni
mwa wiki hii. Wakati wa mashambulizi hayo ya mwezi Septemba mwaka 2013
watu Wasiopungua 67 waliuawa. Tayari ukarabati umefanywa katika jengo
hilo huku wawekezaji katika maduka ya kifahari wakianza kuweka bidhaa
tayari kwa mauzo. Mwandishi wa BBC Abdi Noor Aden amekwenda kuzuru jumba
hilo na kutuletea taarifa ifuatayo.