15 Julai 2015
Wakati
tarehe ya mwisho ya tathmini ya malengo ya maendeleo ya milenia
ikikaribia , nchi ya Tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo zimefanikiwa
kutimiza lengo namba nne linalolenga kupunguza vifo vya watoto walio
chini ya umri wa miaka mitano kwa theluthi mbili. Pamoja na ongezeko
kubwa la idadi ya watu, nchi hiyo imeweza kupunguza asilimia 39 ya vifo
vya watoto. Bila shaka hii ni habari njema lakini bado mapambano
yanaendelea kama anavyotuarifu mwandishi wetu Tulanana Bohela