Tuzo za MTV zimefanyika usiku wa leo, huku zikionekana kutawaliwa na wanigeria,Mwakilishi kutoka Tanzania(Diamond Platnumz) alifanikiwa kuondoka na Tuzo moja ya Best Live act(Mtumbuizaji Bora).
Katika mtandao wa instagram Diamond ameandika “Shukran Kubwa sana Zimfikie Mwenyez Mungu kwa Tuzo hii, na pia Shukran za Dhati Ziwafikie Wadau, Media, Wasanii na Mashabiki zangu wote #TeamWasafi kwa kunipigia kura na Kuhamasisha kwa Nguvu…Niushkuru sana Uongozi wangu, Familia pamoja na Team nzima ya @wcb_wasafi hususan Madancers wangu kwani Naamini wao ndio wamenipika nikapikika hadi leo hii kuweza kuletaTunzo hii Nzito ya Mtumbwizaji Bora Africa, Nyumbani…lakini pia Shukrani za kipekee zimfikie Mama yangu kipenzi Sandra kwa Mafunzo na Malezi anayonipa kila siku juu ya Dunia….na Shukran tena za kipekee na aina yake zimfikie Roho yangu, Kipenzi Changu @zarithebosslady Kwa raha na Usingizi mwanana anipatiao na kunifanya nizidi kutunga na kuwa M’bunifu kwenye kazi.. #BestLiveAct #Mtvmama2015 Asanteni sana “.
Hii ni list ya washindi wote wa MTV AWARDS 2015.
Best Female: Yemi Alade (Nigeria)
Best Male: Davido (Nigeria)
Best Group: P-Square (Nigeria)
Best New Act Transformed by Absolut: Patoranking (Nigeria)
Best Hip Hop: Cassper Nyovest (South Africa)
Best Collaboration : AKA, Burna Boy, Da LES & JR: “All Eyes On Me” (SA/Nigeria)
Song of the Year: Mavins: “Dorobucci” (Nigeria)
Best Live: Diamond Platnumz (Tanzania)
Video of the Year: “Nafukwa” – Riky Rick; Director: Adriaan Louw Best Pop & Alternative: Jeremy Loops (South Africa)
Best Francophone: DJ Arafat (Ivory Coast)
Best Lusophone: Ary (Angola)
Personality of the Year: Trevor Noah (South Africa) MAMA Evolution: D’Banj (Nigeria)
Best International: Nicki Minaj Artist of the Decade: P-Square MTV Base Leadership Award: Saran Kaba Jones & S’Bu Mavundla.http://frankmanyaki.blogspot.com/?zx=b7ab30a0e71f5f92