Siku kadhaa zilizopita mkurugenzi wa jiji la mwanza alifanya kikao akiwa na mkuu wa wilaya ya nyamaghana na wenyeviti wote wa serikali zamitaa katika jiji la mwanza .
na kuwataka wenyeviti wote warudishe mihuli na wakabidhiwe watendaji kwa kile kinachodaiwa kuwa wanakiuka makubaliano na kutumia mihuli hiyo kwa njia ambayo siyo ya halali,
lkn matokeo yake wenyeviti hao walikuja juu na kugoma kurudisha mihuli na kumtaka rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania ndugu magufuli kumfukuza kazi mara moja.
kikiwa kimya bado hatuja pata hatma ya sekeseke hilo.
leo usiku katika malumbano ya hoja yanayorushwa moja kwa moja toka ITV NA CAPITAL RADIO NA RADIO ONE STEREO kuanzia saa tatu mpka tano usiku ambao walikuwa wanamuhoji makamu mkurugenzi ofisi ya waziri mkuu tamisemi.wachangiaji ambao wengi walikuwa ni wenye viti wa mtaa wameonekana kukerwa na kitendo cha mkurugenzi huyo na serikali kwa ujumla na kuomba nje ya kuachiwa mihuli wapewe mishahara kama ilivyo kwa wabunge na watumishi wengine wa serikali.
wachangiaji wengine wakaenda mbali zaidi wakasema kama watanyanganywa mihuli basi hata na rais naye hataruhusiwa kuwa na mihuli,ifike mda tutofautishe kati ya kiongozi na mtendaji wa eneo husika kazi kwa viongozi wenye dhaman ya kuliondoa jambo hili