C.E.O wa lebo ya WCB Wasafi Diamond Platnumz amefunguka sababu zilizomsukuma yeye kufungua lebo ya muziki na kusimamia wasanii wake na kuhakikisha wanafika mbali.
ADiamond Platnumz amedai kuwa ni u-snitch wa wasanii wenzake ndio sababu kubwa ambayo ilimpa hasira na kuamua kuanzisha lebo yake kutokana na wasanii hao kutokuwa na msimamo na nguvu moja katika kuhakikisha wanaupa thamani muziki wanaoufanya na kuhakikisha unafika mbali.
“Point kubwa kabisa kwangu mimi iliyonisukuma kuanzisha lebo yangu ni kutokana na utengano, usnitch, kusengenyana kati ya wasanii na wasanii, kulikuwa hakuna ushirikiano wala umoja. Ilikuwa hata kama nikiwa na wazo nikimfikishia mwenzangu ili tufanye muziki wetu uweze kufika mbali anashindwa kuniamini na kudhani kwamba nampangia njama za kumuangusha. Na huwezi kufika mbali kisanaa wewe kama wewe ni lazima muwe wengi, na wengi waliokuwa na malengo ya kufika mbali walikuwa hawana malengo ya kutaka muziki wa Tanzania ukue. bali walikuwa wanataka kunifunika. Nikaona isiwe kesi nikaamua kutengeneza watu wangu ambao lengo letu litakuwa ni moja katika kushirikiana kuipeleka sanaa ya Tanzania mbali.”
Hayo ni machache kati ya mengi ambayo ameyazungumza Diamond Platnumz katika interview Kuitazama interview nzima play hii video hapa chini.