Mwanamama mmoja ambaye ni mfuasi wa chama cha Democratic ambaye alivunjwa moyo na kushindwa na Bi Hillary Clinton amekutana na mtu na Bi clinton porini bila kutegemea.
Margot Gerster alienda matembezi akiwa na binti yake na mbwa katika msitu wa Chappaqua, New York.
Hakutarajia kukutana na Bi Clinton ambaye alishindwa na Donald Trump wa Republican siku mbili zilizopita, lakini hilo ndilo lililotokea.
inasemekana kuwa picha hii ndiyo ya kwanza kumuonyesha bi hillary clinton tangu kumaliza kwa uchaguzi wa marekani na yeye kusindwa vibaya na bwana trump.
Ingali yeye mwenyewe bibi clinton amesema trump apewe sifa ya kuongoza lkn bado kumekuweko na maandamano ya kupinga ushindi wa trump toka kwa wakazi wa nchi hiyo ya marekani.
Bi Gerster, ambaye huishi White Plains, amesimulia kuhusu kisa hicho kwenye Facebook.
Ujumbe wake ulipendwa mara zaidi ya 110,000 na kusambazwa na watu 9,000 kabla yake kuufanya wa faraghani.
"Nilimkumbatia na kuzungumza naye na kumwambia kwamba moja ya nyakati ninazojivunia zaidi kama mama ni wakati ambao nilimbeba Phoebe nikaenda naye na tukampigia kura," amesema.
"Alinikumbatia na kunishukuru na tukasemezana na kisha nikamwacha aendelee na matembezi."
Bi Clinton na mumewe huishi Chappaqua, wilaya ya Westchester, na ni eneo hilo ambapo Bi Clinton alipiga kura Jumanne.
Na haionekani kana kwamba hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Bi Gerster kukutana na waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje.
Alipakia mtandaoni picha yake na Bi CLinton, ambaye anasema alipigwa picha naye alipokuwa shule ya pili, wakati wa hafla ya kuchangisha pesa iliyoandaliwa na mamake.