manyaki-1.jpg ...      ...

MSHAMBULIAJI AJERUHI NA KUUA ZAIDI YA WATU 11 OHIO MAREKANI

Mwanafunzi wa kisomali kwenye chuo kikuu cha Ohio ameendesha gari yake kwenye mkusanyiko wa watembea kwa miguu Jumatatu na halafu kutoka nje ya gari na kuanza kuwachoma visu, akijeruhi watu 11.
Alipigwa risasi na kuuawa na polisi. Mkuu wa polisi wa Columbus, Kim Jacobs amesema wanaliona shambulizi hilo kuwa ni kitendo cha kigaidi.
Chuo kikuu cha Ohio kimemtaja mshambuliaji kuwa ni Abdul Razak Ali Artan, mwanafunzi katika chuo hicho. Wana jumuiya katika mji wa Columbus wameiambia VOA kuwa mwanamme huyo mwenye asili ya kisomali alikuwa na umri wa miaka 20.
Mwanafunzi mwenye jina kama hilo katika chuo hicho aliwahi kutajwa katika toleo la mwezi Agosti la gazeti la chuoni hapo akielezea wasi wasi wa kutokuwepo kwa vyumba vya kufanya ibada kwenye chuo kikuu hicho.
Maafisa hospitali wamesema hakuna muathirika aliyepata majeraha ya kutishia maisha yake. Rais wa chuo kikuu Michael Drake amesema kulikuwa na uvumi wa mshukiwa wa pili. Hata hivyo, Drake amesema polisi walifanya msako na wanaamini kulikuwa na mshambuliaji mmoja tu. Shirika la Upelelezi la FBI limejiunga katika  uchunguzi.
Previous
Next Post »