Wananchi wa marekani na wanaharakati wa kutetea haki za kiraia yamemuomba rais wa marekani Barack Obama kuivunja program ambayo iliwahi kutumika kuandikisha wageni kutoka nchi kadhaa za kiislamu.
Ikumbukwe kuwa kampeni hiyo iliwekwa hili kuweka vizuizi vya rais ajaye bwana trump kama ishara ya kupinga Sera yake ya kuwazuia waislamu nchini kwake.
Katika barua yao kwa Obama ambayo imebandikwa katika mtandao Jumanne, taasisi 198 za ndani na za kitaifa za Marekani zimetaka hatua za kiutendaji zichukuliwe haraka.
Hatua hizo ni kubatilitisha mfumo wa usalama wa taifa wa kuandikisha wageni wanaoingia na kutoka ambao unajulikana kama NSEERS.
NSEERS ilikuwa ni sera ya kibaguzi ambayo ilienda kinyume na misingi ya Marekani ya haki na usawa kwa wote.
Barua ya kundi hilo imeandika na kuongezea kwamba ulikuwa haikuwa nyenzo muafaka kukabiliana na ugaidi, na kupelekea athari nyingi kwa watu binafsi ambao waliathiriwa moja kwa moja na kuvuruga uhusiano na jamii za wahamiaji.