Taarifa iliyotolewa leo November 17 2016 kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametia saini Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 iliyopitishwa na Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wake wa 5 Mjini Dodoma.
Rais Magufuli amesaini Sheria hiyo tarehe 16 Novemba, 2016. Dkt. Magufuli amewapongeza wadau wote kwa kufanikisha kutungwa kwa Sheria hiyo.Baada ya kusaini mkataba huo Rais Amesema"Naamini kuwa Sheria hii itasaidia kuboresha sekta ya habari kwa manufaa ya wanataaluma wenyewe na Taifa"