Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Ijumaa aliongoza baraza lake la mawaziri kwa mkutano maalum ambao unafanyika katika ikulu dogo ya Sagana State Lodge, nje ya mji wa Nairobi, ambao, kulingana na taarifa kutoka ikulu, unajadili jinsi ya kutekeleza kwa haraka miradi ambayo muungano unaotawala wa Jubilee, uliwaahidi wapigaji kura wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi wa mwaka wa 2013.
Haya yanajiri wakati utawala wa rais Kenyatta ukikabiliwa na shutuma kali za baadhi ya maafisa wake kuhusika kwa ulaji rushwa, pamoja pia na tuhuma kwamba mengi ya makubaliano yaliyoafikiwa kwenye mikutano kama hiyo, bado hayajatekelezwa.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya, mkutano huo unatarajiwa kutadhmini yale ambayo serikali imetekeleza kufikia sasa, na mwelekeo wa mikakati yake, kwelelekea kwa uchaguzi mkuu wa Agosti mwakani.