Meli ya Titanic iliyojengwa na Harland na Wolff huko Belfast,
iligonga mwamba wa barafu na kuzama Kaskazini mwa Atlantic mwaka 1912 na
kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,500 ilikuwa katika safari yake
kutoka Southampton ikielekea New York.
Leo ikiwa
ni takribani mia na nne imepita tangu meli hiyo izame, China wameamua
kujenga meli inayofanana na Titanic, habari kuhusu meli hiyo
imewashangaza raia wengi waChina. Ujenzi huo wa meli hiyo yenye urefu wa
kina cha mita 269 umeanza
Meli hiyo
ya China, itakuwa yenye umbo sawa na ile ya Titanic , itakuwa na sehemu
ya michezo, maonyesho, kuogelea na sehemu maalum ya watu maalum ambayo
itakuwa na mtandao wa Wifi na inatarajiwa kuwa kivutio kikubwa katika
eneo hilo la theme park lililoko kilomita kadhaa kutoka pwani ya China.