Wapiga kura katika taifa la magharibi mwa Afrika Gambia wanaelekea katika uchaguzi ambao rais aliyepo mamlakani Yahya Jammeh anasema kuwa atashinda.
Rais Jammeh ambaye alichukua mamlaka katika mapinduzi ya mwaka 1994 anasema kuwa ataongoza kwa miaka bilioni Allah akipenda.
Akiwania wadhfa huo kwa muhula wa tano amesema kuwa anapiga marufuku maandamano baada ya uchaguzi huo kwa sababu ni vigumu kufanya udanganyifu.
Mpinzani mkuu wa Jammeh ni mwanasiasa aliyejiingiza katika uchaguzi huo hivi majuzi Adama Barrow ambaye anaongoza muungano wa upinzani.
Viongozi kadhaa wa upinzani wanahudumia vifungo jela baada ya kushiriki katika maandamano yasio ya kawaida mwezi Aprili.
Pamoja na hayo yote rais Jammeh amejinasibu kuwa hatishwi na jambo lolote katika uchaguzi huo wakati huo huo wapinzani wake wanadai tabia zisizofaa
zimemuandama rais huyo miezi kadhaa iliyopita kabla ya kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho.
Upande wa upinzani umekuwa ukipiga kampeni kwa nguvu zao zote katika siku za hivi karibuni, ingawa mpaka sasa viongozi wakuu wa vyama vya upinzani wako magerezani baada ya kufanya maandamano katika mitaa mbali mbali ya jiji la Gambia mnamo mwezi wa nne mwaka huu.
Mpaka sasa inaarifiwa kuwa serikali ya Gambia imekata mawasiliano yote ya simu ikiwemo mitandao huku wapinzani