Mtuhumiwa wa ujangili Yusufu Ally Maarufu kwa jina la mpemba pamoja na wenzake watano walipandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu Dar es salaam November 16 kusomewa mashitaka manne yanayowakabili.
Leo December 1 2016 kesi hiyo imetajwa ambapo watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo, wakili wa upande wa Jamhuri Patrick Mwita aliimbia mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilikka, awali November 16 2016 watuhumiwa hao walipofikishwa mahakamani hapo upande wa jamhuri ulisema upelelezi umekamilika,
Kesi hiyo itatajwa tena December 15 2016, hakimu mkazi mwandamizi, Thomas Simba amewataka upande wa Jamhuri watakapokuja December 15 2016 kesi hiyo upelelezi uwe umekamilika.