KISOMO cha kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa mwimbaji
mahiri nchini, marehemu Amina Ngaluma ‘Japanese’ kinatarajiwa kufanyika
Jumamosi wiki hii Kitunda, Machimbo Dar es Salaam.* Akizungumza baba mzazi wa marehemu, Kassim Ngaluma, alisema kisomo hicho
kitafanyika nyumbani kwa wazazi wake marehemu na kuwaomba ndugu, jamaa na
marafiki mbalimbali wa marehemu wakati wa uhai wake wahudhurie.“Tunaomba wote tulioshiriki kwa namna mbalimbali wakati wa msiba wa
marehemu mwanangu, tushirikiane pia katika kumbukumbu ya mwaka mmoja wa
kifo chake,” alisema Mzee Ngaluma.
Amina Ngaluma ‘Japanese’ ENZI ZA UHAI WAKE