manyaki-1.jpg ...      ...

PICHA:MTAZAME NAIBU WAZIRI WA AJIRA KAZI NA ULEMAVU AKICHIMBA MSINGI NA WANANCHI WAKE.

Naibu waziri wa Kazi ajira na Walemavu Mhe.Anthony Mavunde ambaye ni mbunge wa Dodoma Mjini akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Muungano ambapo amefanya ziara ya kushtukiza kwa wananchi wake kuangalia shughuli mbalimbali za maendeleo 
 Alipotembelea kijiji cha Muungano Mbalawala na kuwakuta wakichimba msingi wa kujenga madarasa ameshirikiana nao kitu kilichowashangaza wananchi walio wengi kuona mbunge wao akishika sururu na kuanza kuchimba msingi nao na kuwaambia nachimba  huu msingi ikiwa ni moja ya kazi nilizoahidi kuzifanya wakati nikiomba kura za ubunge jimbo la dodoma mjini hapa kwenu.
 Kijana akimpokea Waziri Mavunde Surur ambapo waziri huyo amekataa na kuendelea nao hadi walipomaliza jioni kuchimba msingi huo wa vyumba vya madarasa


Masama Blog ilimuuliza waziri Mavunde kwa nini ameamua kuchimba msingi badala ya kuwaachia mafundi waendelee na kazi yao hiyo?...Naye akajibu hivi...''Leo nimeshiriki pamoja na wananchi wa kijiji cha Muungano kata ya Mbalawala katika ujenzi wa shule ya msingi Muungano katika kuunga mkono juhudi za wananchi na pia katika kutekeleza ahadi zangu kama Mbunge nimewachangia mifuko 50 ya saruji 
Previous
Next Post »