Msanii na mwanamitindo Jokate Mwegelo amefunguka na kusema kuwa amegundua katika maisha ya mahusiano ya mapenzi huwa anavutiwa na kuwapenda sana wanaume ambao ni wapole na wale wasiokuwa na mbwembwe na majivuno.
Jokate Mwegelo amesema hayo kupitia katika ya ‘Account’ yake ya Twitter ambapo alikuwa akijibu baadhi ya maswali ambayo alikuwa anaulizwa na mashabiki zake kupitia mtandao huo.
Jokate anasema anapenda wanaume ambao wako ‘busy’ kwenye kazi zao na biashara zao na wale ambao wanajali.
“Nimegundua napenda wanaume wapole as in wasiokuwa na mashamsham, matashtiti ila firm kwenye kazi zao na wanaojali” aliandika Jokate
Mbali na hilo Jokate alisema anatamani kuwa mwanasiasa na kama ikitokea nafasi hiyo anaweza kuwa mwanasiasa kwani yeye toka akiwa mdogo alikuwa anapenda sana watu pamoja na maendeleo yao.
“Watu wengi wanaona hilo kwangu. kiukweli napenda sana watu na maendeleo yao, tangia mdogo niko hivyo so itategemea na nafasi itakapotokea” alisema Jokate