Ni mwanafunzi mmoja pekee nchini Liberia kati ya wanafunzi 42,000 waliokalia mtihani wa kila mwaka wa eneo la Afrika Magharibi aliyepita mtihani huo ili kujiunga na chuo kikuu.
Armstrong Gbessagee mwenye umri wa miaka 18 kutoka chuo cha J.J Roberts United Methodist mjini Monrovia ndiye mwanafunzi wa pekee aliyefaulu.
Amstrong alisema: Kokote unakotoka haimaanishi kwamba wewe sio mwerevu ukilinganishwa na watu wengine wa Afrika Magharibi.Natumai wengine wanaona ufanisi wangu kuwa motisha.
Mitihani hiyo hufanyika nchini Ghana,Nigeria,Sierra Leone,Liberia na Gambia, mataifa yanayozungumza kiingereza.
Mwaka 2013 takriban wanafunzi 25,000 walifeli mtihani huo wa kujiunga na chuo kikuu cha Liberia,ikiwa ni mojawapo ya vyuo vikuu vinavyoendeshwa na serikali.
Rais wa Liberia Ellen Sirleaf Johnson aliitaja sekta ya elimu kuwa na tatizo.